Timu Yetu

DW yawaletea Bundesliga Jumamosi "Live"

Moja kwa moja kutoka nyumbani kwa mabingwa wa soka wa dunia, Ligi ya Ujerumani, Bundesliga, inakujia sasa nyumbani kwako barani Afrika kupitia radio Deutsche Welle na washirika wake.

Kila Jumamosi  Idhaa ya Kiswahili ya DW inakuletea  pambano  la  kukata  na  shoka  la  ligi ya Ujerumani Bundesliga  ambapo tunakuchagulia pambano  ambalo linavutia  kwa  vigezo maalumu.

Jumamosi hii (09.12.2017) tumekuchagulia mchezo  kati ya  Eintracht Frankfurt na  Bayern Munich utakaochezwa katika uwanja wa Commerzbank-Arena.

Bundesliga Hertha BSC - Eintracht Frankfurt Boateng Tor (picture-alliance/dpa/A. Hilse)

 

Bayern inashikilia nafasi ya 1 ikiwa na  pointi 32 wakati Frankfurt ikiwa katika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 22. 

Kwa hisia na vitendo kutoka kwa baadhi ya wachezaji bora duniani, Bundesliga itakuwa na kila kitu cha kukufurahisha ikiwa ni pamoja na taarifa muhimu za wachezaji. Nchi wanazotoka, wamecheza mara ngapi katika Bundesliga na kadhalika.

Bundesliga - Bayern München vs Hannover 96 (Reuters/M. Dalder )

Katika Deutsche Welle Bundesliga Live, unaweza sasa kusikiliza mapambano hayo kwa Kiswahili. Jiunge nasi kila Jumamosi saa 11.25  jioni kwa saa za Afrika mashariki, ili kupata matangazo hayo ya Bundesliga Live.

Sikiliza sauti

Kutana na watangazaji wako Sekione Kitojo, Josephat Charo, Bruce Amani, Jacob Safari na Isaac Gamba wakiwa na mchambuzi aliyebobea katika Bundesliga, Ramadhan Ali.

Washirika wetu

Unaweza kusikiliza matangazo haya kupitia redio washirika wetu Afrika mashariki na kati.
Nchini Tanzania kupitia:


Dar es Salaam: Capital FM, Mlimani FM, Wapo Radio
Mkoani Kagera: Fadeco Community Radio na Kasibante FM Radio
Tanga: Mwambao FM
Mwanza: Radio Free Africa na Radio SAUT FM STEREO na Kiss Fm
Mtwara: Pride FM na Safari FM
Mbeya: Ushindi Radio
Arusha: Triple A FM
Moshi: Radio Sauti ya Injili
Mpanda: Mpanda FM Radio
Kahama: Kahama FM
Iringa: Overcomers FM

Kenya washirika wetu ni:
Nairobi: Radio Maisha
Webuye: Radio Mambo
Lamu: Sifa FM
Kapenguria: North Rift Radio

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo:
Uvira:  Radio Ondese
Bunia:RTM
Lubumbashi: Radio Phoenix
 

Uganda washirika wetu ni:
Tororo: Veros Radio
Mbale: Signal FM

Na kupitia satalaiti: SES-5 na Eutelsat 5W

Matangazo ya moja kwa moja katika mtandao wa intaneti unaweza kuyasikia ukibonyeza link chini. Ni wakati matangazo yakiwa yanaendelea tu.

Viungo vya WWW

Albanian Shqip

Amharic አማርኛ

Arabic العربية

Bengali বাংলা

Bosnian B/H/S

Bulgarian Български

Chinese (Simplified) 简

Chinese (Traditional) 繁

Croatian Hrvatski

Dari دری

English English

French Français

German Deutsch

Greek Ελληνικά

Hausa Hausa

Hindi हिन्दी

Indonesian Bahasa Indonesia

Kiswahili Kiswahili

Macedonian Македонски

Pashto پښتو

Persian فارسی

Polish Polski

Portuguese Português para África

Portuguese Português do Brasil

Romanian Română

Russian Русский

Serbian Српски/Srpski

Spanish Español

Turkish Türkçe

Ukrainian Українська

Urdu اردو