1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ehud Barack akutana na rais Mubarak,Misri

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgNj

CAIRO

Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barack anazuru Misri leo hii ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipochaguliwa katika wadhifa huo mwezi juni.Ehud Barack atakuwa na mazungumzo na rais Hosni Mubarak wa Misri na maafisa wengine wa ngazi ya juu wanaohusika na usalama.Mkutano huo utakaofanyika katika eneo la kitalii la Sharm El Sheikh unakuja wakati kukiwa na mivutano juu ya madai uingizwaji wa silaha kimagendo katika Gaza.Katika kikao cha leo waziri wa ulinzi wa Israel anatarajiwa kuitaka Misri kuzuia shughuli hiyo ya uingizaji wa silaha katika ukanda wa Gaza kutoka eneo la Sinai.Eneo la Gaza kwa sasa linasimamiwa na kundi la Hamas ambalo linaangaliwa kama kundi la kigaidi na Israel na mataifa ya magharibi.Misri imekuwa na jukumu muhimu katika mazungumzo ya kumkomboa mwanajeshi wa Israel Gilad Shalit anayezuiliwa mateka na wanamgambo wa Gaza tangu mwezi Juni mwaka jana.Aidha inaaminika kwamba Israel huenda ikaawaachia huru wafungwa 450 wakipalestina ili Gilad Shalit aachiwe huru.