1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ehud Barak kukutana na rais Mubarak mjini Cairo

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfEV

Waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Barak, anajiandaa kukutana na rais wa Misri, Hosni Mubarak katika siku chache zijazo mjini Cairo.

Mshauri wa maswala ya siasa wa wizara ya ulinzi ya Israel, jenerali Amos Gilad, amesema Ehud Barak atasafiri kwenda Cairo kuzungumza na rais Mubarak juu ya maswala ya usalama na maswala mengine muhimu.

Hata hiyo jenerali Gilad amesema viongozi hao hawatajadili uwezekano wa kufanya makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la Hamas linalolitawala eneo la Ukanda wa Gaza.

Kundi la Hamas leo limeanza kuandaa kanuni za kufanya mkataba wa kusitisha mapigano na Israel huku likijaribu kutafuta kuungwa mkono na makundi mengine ya wanamgambo wa kipalestina.

Wakati haya yakiarifiwa wapalestina wawili wamejeruhiwa leo kufuatia shambulizi la kombora lililofanywa karibu na kivuko cha mpakani cha Karni.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema hana habari kuhusu operesheni ya kijeshi katika eneo hilo hivyo kuashiria huenda shambulizi hilo limefanywa kimakosa na wanamgambo wa kipaesltina.