1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eliud Kipchoge ashinda London Marathon

Sekione Kitojo
23 Aprili 2018

Eliud Kipchoge wa Kenya ameshinda mbio ndefu za London Marathon kwa mara ya tatu. Alishinda katika mwaka wa 2015 na 2016

https://p.dw.com/p/2wWjY
UK London Marathon 2018 | Gewinner Eliud Kipchoge und Vivian Cheruiyot aus Kenia
Picha: picture-alliance/Xinhua/R. Washbrooke

Bingwa  wa  Olimpiki Eliud Kipchoge  ameshinda  taji  lake  la  tatu  la mbio ndefu marathon mjini  London  jana  Jumapili  na  kukamilisha ushindi  mara  mbili  wa  Wakenya  baada  ya  Vivian Cheruiyot kushinda   mbio  hizo  kwa  upande  wa  wanawake.

Kipchoge mwenye  umri  wa  miaka  33, alimshinda  Muithiopia  Tola Shura pamoja  na  Mo Farah  wa  Uingereza  na  kushinda  mbio  zake  za tatu  za  London Marathon  kwa  kutumia  muda  wa  masaa  2 dakika 4  na  sekunde  17, akimaliza  zaidi  ya  nusu  dakika  mbele  ya Kitata na Mo Farah  akiwa  wa  tatu  kwa  kutumia  masaa  2  dakika 21  na  sekunde 40.

Eliud Kipchoge kenianischer Marathonläufer
Eliud Kipchoge wa KenyaPicha: Imago/Hindustan Times

"Hii  ni  siku  kubwa  kwangu. Kushinda  London  Marathon  na mashindano  ya  dunia. Ni  mkusanyiko wa mataji  mawili. Najisikia vizuri sana."

Nayo  kamati  ya  kimataifa  ya  Olimpiki  IOC leo  imewataka viongozi  wa  mji  wa  Tokyo, ambao  ndio  utakuwa  mji utakaotayarisha  mashindano  ya  mwaka  2020  ya  olimiki kujitayarisha  kwa  uchunguzi  zaidi  baada  ya  mafanikio  makubwa ya  mashindano  ya  majira  ya  baridi  yaliyofanyika  mjini Pyeongchang Korea  kusini.

Wakati  wa  mradi  wa  mapitio  wa  siku mbili  kwa  ajili  ya  olimpiki  ya  mwaka  2020, makamu  wa  rais  wa IOC John Coates  aliweka  mbinyo kwa  Tokyo  kutayarisha mashindano  yenye  mafanikio  katika  muda  wa  miaka  miwili kuanzia  sasa.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / afpe / rtre

Mhariri: Yusuf , Saumu