1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Enzi ya Edmund Stoiber yamalizika

P.Martin29 Septemba 2007

Wahafidhina katika jimbo la Bavaria,kusini mwa Ujerumani hii leo wanamchagua mrithi wa Edmund Stoiber kama mwenyekiti wa chama cha Christian Social Union-CSU.

https://p.dw.com/p/CB0r
Waziri Mkuu wa Jimbo la Bavaria,Edmund Stoiber baada ya kuhotubia mkutano mkuu wa chama chake cha CSU mjini Munich
Waziri Mkuu wa Jimbo la Bavaria,Edmund Stoiber baada ya kuhotubia mkutano mkuu wa chama chake cha CSU mjini MunichPicha: AP

Stoiber pia anamaliza awamu ya miaka 14 kama waziri mkuu wa jimbo la Bavaria,baada ya kushinikizwa na wanachama wenzake kwa miezi kadhaa.

Uongozi wa chama cha CSU unagombewa na wanachama watatu:Waziri wa Uchumi wa Bavaria,Erwin Huber;Waziri wa Kilimo wa Ujerumani,Horst Seehofer na Gabriele Pauli ambae juma lililopita alihoji maadili ya chama hicho,kuhusu masuala ya familia.Bibi Pauli alishauri kuwa ndoa zidumu kipindi cha miaka saba.

Günther Beckstein ambae hivi sasa ni Waziri wa Ndani wa jimbo la Bavaria,anamrithi Stoiber kama waziri mkuu wa jimbo hilo.