1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Erdogan asema Uturuki inaliunga mkono kundi la Hamas

Tatu Karema
9 Machi 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema leo kuwa nchi yake inaliunga mkono kikamilifu kundi la wanamgambo la Hamas

https://p.dw.com/p/4dL0y
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akihutubia katika mkutano wa kisiasa mjini Ankara mnamo Januari 18, 2024
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Adem Altan/AFP/Getty Images

Katika taarifa aliyotoa mjini Instabul, Erdogan amesema hakuna anayeweza kuwashawishi kuliorodhesha kundi la Hamas kama la kigaidi na kwamba Uturuki ni taifa linalowasiliana kwa njia za wazi na viongozi wa kundi hilo.

Soma pia:Erdogan ahutubia maandamano ya kuiunga mkono Palestina

Erdogan ni mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israel tangu kuanza kwa vita katika ukanda huo wa Gaza. Amekaririwa mara kadhaa akiukosoa utawala wa Israel na kuushutumu kwa kufanya kile amekiita "mauaji ya kimbari" kwenye Ukanda wa Gaza

Vita vyaGazavilizuka baada ya shambulizi la kushtukiza la Hamas Kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7 ambavyo Israel inadai vimesababisha vifo vya takriban watu 1160.

Soma pia:Erdogan na Netanyahu wakutana kwa mara ya kwanza tangu mahusiano kuingia doa

Israel imejibu shambulizi hilo la Hamas kwa mashambulizi mfululizo ya ardhini na angani ambayo wizara ya afya inayosimamiwa na kundi hilo la Hamas katika ukanda huo wa Gaza imesema hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 30,878.