1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Leclerc arejesha tabasamu kwa ushindi wa Austria

Bruce Amani
11 Julai 2022

Mfaransa Charles Leclerc alirejesha tabasamu baada ya kushinda mbio za Austrian Grand Prix kwa kumpiku dereva wa Red Bull Max Verstappen. Carlos Sainz alilazimika kujiondoa baada ya kukumbwa na matatizo ya injini

https://p.dw.com/p/4DyTO
Formel 1 Großer Preis von Österreich | Sieger Charles Leclerc, Ferrari
Picha: Johann Groder/AFP/Getty Images

Charles Leclerc alipambana kumpiku Max Verstappen na kuchukua ubingwa wa Austrian Grand Prix Jumapili na kuyafufua matumaini yake ya ubingwa wa ulimwengu lakini matumaini ya Ferrari kumaliza nafasi ya kwanza na pili yaliungua.

Wakati Leclerc alipata ushindi wake wa kwanza katika mashindano saba mfululizo mwenzake wa Ferrari Carlos Sainz alilazimika kujiondoa mashindanoni baada ya gari lake kuwaka moto kutokana na matatizo ya injini.

Lewis Hamilton alimaliza katikan nafasi ya tatu mbele ya mwenzake wa timu ya Mercedes George Russel. Ni ushindi wa tatu wa Leclerc mwaka huu na wa kwanza wa Ferrari katika mzunguko wa Red Bull Ring tangu Michael Schumacher mwaka wa 2003.

ap