1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Farah alenga kuweka kando masaibu yake

20 Juni 2015

Bingwa mara mbili wa olimpiki Mo Farah amedhibitisha atarudi tena katika mashindano ya riadha yanayojulikana kama Diamond League huko Monaco Julai 17

https://p.dw.com/p/1Fk4Y
Leichtathletik WM Moskau Mo Farah
Picha: Reuters

Farah atashiriki mashindano mara ya kwanza tokea yalipotolewa madai ya kutumia madawa ya kuimarisha nguvu . taarifa ya kurejea kwake katika mashindano hayo ilitangazwa na kocha wake Alberto Salazar.

Farah, raia wa Uingereza mzaliwa wa Somalia mwenye umri wa miaka 32 alijitoa katika mashindano ya Birmingham mapema mwezi huu kutokana na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya Salazar na kocha msaidizi Galen Rupp. Wote wawili wamekanusha madai hayo. Wakati Farah binafsi hakushutumiwa kwamba ametenda lolote lililo kinyume na sheria, mwanariadha huyo amesema atakuwa bega kwa bega na kocha wake huyo Mmarekani hadi imethiobitishwa kuwa ni mkosa.

Bingwa huyo mara tatu wa dunia amesharejea kutoka Marekani, ili kuanza mazoezi nchini Ufaransa kabla ya mashindano hayo ya riadha ya Monaco. Wiki moja baadae Farah anatarajiwab kushiriki katika mashindano yanayojulikana kama Annivesary Games katika uwanja wa Olimpik mjini London. Chini ya ukufunzi wa Salazar , mwanariadha huyo ameshinda mataji matano ya dunia katika mbio za mita 5,000 na 10,000

Mwandishi:Mohammed Abdul-Rahman,rtr,afp,dpa,ap
Mhariri:Josephat Charo