1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Faure Gnassingbe ametangazwa mshindi kwenye duru ya kwanza

Saleh Mwanamilongo
24 Februari 2020

Faure Gnassingbe aliewania muhula wa nne ametangazwa mshindi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo,ambao ulikuwa na wagombea saba.Upinzani tayari umelalamikia matokeo hayo

https://p.dw.com/p/3YHoh
Rais wa Togo faure Gnassingbe achaguliwa kwa muhula wa nne
Rais wa Togo faure Gnassingbe achaguliwa kwa muhula wa nnePicha: Getty Images/C. Marquardt

 Tume huru ya uchaguzi nchini Togo imemtangaza rais Faure Gnassingbe kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Juma mosi iliopita, baada ya kupata asimilia 72.3 za kura, huku mgombea wa upinzani na waziri mkuu wa zamani Agbeyome Kodjo alieoko katika nafasi pili kwa asilimia 18.3 akipinga matokeo hayo kwa madai kwamba kulikuwepo na wizi wa kura. Koti ya katiba inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo ya uchaguzi mnamo kipindi cha wiki moja.

Rais Gnassingbe aliewania muhula wa nne ametangazwa mshindi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo,ambao ulikuwa na wagombea saba.

Togo Lome Anhänger von Präsident Gnassingbe
Picha: Reuters/L. Gnago

Upinzani ambao uliahaidi kuunga mkono mgombea mmoja kwa duru ya pili tayari umelalamikia matokeo hayo yaliotangazwa mapema leo juma tatu.

Agbeyome Kodjo, mshindi wa pili amepata asilimia 18 nukta 3 pekee za kura, na nafasi ya tatu ilishikiliwa na mpinzani mkongwe wa utawala wa Gnassingbe, Jean-Pierre fabre ambae alipata asilimia 4 nukta 3 za kura. Wagombea wengine 4 hawakufikisha asilimia moja ya kura.

Waziri wa ajira na  mtu wa karibu wa rais Gnassingbe alielezea ameliambia shirika la AFP kwamba ni kwa mara ya kwanza mgombea wa chama chao kupata ushindi kama huo. Miaka mitano iliopita rais Faure Gnassingbe alichaguliwa kwa asilimia 58.

''Leo tumeona kwamba rais Faure Gnassingbe amefanya vizuri sana kwenye majimbo ambayo hayakumpigia kura kwenye chaguzi zilizopita'' alisema Bawara baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ni kwamba watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 76 nukta 6. Idadi hiyo ni kubwa kuliko mwaka 2015 ambapo ilikuwa ni asilimia 60. Kwa mara ya kwanza pia matokeo yametangzwa mapema kuliko chaguzi zilizopita.Kwa ujumla uchaguzi wa juma mosi ulifanyika katika hali ya utulivu.

Kasoro za uchaguzi

Masaa kadhaa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, mpinzani ambae hakutarajiwa Agbeyome Kodjo,waziri mkuu wa zamani na spika wa bunge la Togo,alijitangaza kuwa mshindi wa uchaguzi ,na hiyo kujiita kuwa ''rais aliechaguliwa kidemokrasia''.

Agbeyome Kodjo  mgombea wa upinzani Togo
Agbeyome Kodjo mgombea wa upinzani TogoPicha: Reuters/L. Gnago

''Kama rais aliechaguliwa kidemokrasia nimeahidi kuunda serikali mnmo siku za usoni ambayo itashirikisha pande zote'',alisema Kodjo.

Huku akimtolea wito rais Faure Gnassingbe kuonesha 'uzalendo na kukabidhi madaraka kwa amani.

 Faure Gnassingbev alishika madaraka mwaka 2005 kufuatia kufariki baba yake,jenerali Gnassingbe Eyadema,ambae aliongoza nchi hiyo ndogo ya afrika ya magharibi kwa kipindi cha  miaka 38.

Hivi sasa Faure Gnassingbe amechaguliwa kwa muhula wa nne,baada ya mihula mitatu ambayo matokeo ya uchaguzi yalighubikwa na tuhuma za wizi wa kura.

Licha ya kwamba uchaguzi ulifanyika katika hali ya utulivu, lakini mashirika ya kiraia nchini humo yalielezea kwamba kwenye baadhi ya vituo wawakilisji wa upinzani hawakuruhusiwa, na mtandao wa intaneti pia ulikatwa kwa mara kadhaaa hiyo juma mosi.

 Makaazi ya mgombea wa upinzani Kodjo na mshirika wake ambae ni askovu wa zamani wa mji wa mji mkuu wa  Lome,yalizingirwa na polisi kwa masaa kadhaa usiku wa kuamkia juma pili.