1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FC St.Pauli

Ramadhan Ali20 Juni 2007

FC St.Pauli -klabu ya daraja ya pili ya Bundesliga iliasisiwa 1910 na 2001 ilipanda daraja ya kwanza . Msimu ujao itarejea daraja ya pili kutoka ya tatu.

https://p.dw.com/p/CHbv

FC Sankt Pauli ni timu ya pili ya Hamburg.Maarufu zaidi mjini humo ni Hamburger SV-mabingwa mara kadhaa wa Ujerumani na hasa walipocheza na muingereza Kevin Keegan na Franz Beckenbauer.Muafrika alietamba na Hamburg alikua mghana Anthony Yeboah.

FC St.Pauli,timu ya Millerntor, imekua ikiyumba yumba kati ya daraja ya kwanza na ya pili na hata ya tatu.Baada ya miaka 4 katika Ligi ya mkoa ya kaskazini au ya daraja ya 3 msimu ujao FC st.Pauli inarudi daraja ya pili ya Bundesliga.

Ramadhan Ali anasimulia FC st.Pauli:

“Mpira umekwisha,mpira umemalizika saa 3 na dakika 32 za usku wa ijumaa hii ya tarehe 25 mei.FC st.Pauli imepanda daraja ya pili ya Bundesliga.”

Miaka 4 mashabiki wa St.Pauli wakistahimi hadi kupanda tena timu yao daraja ya pili.Mapenzi ya mashabiki wake St.Pauli hayatokani tu na kushinda ,kwani St.Pauli haikuwahi kutawazwa mabingwa wa Ujerumani katika historia yake wala haikuwahi kutwaa kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani seuze kombe la ulaya.

Mnamo miaka ya 1980 klabu hii iliinuliwa na vijana chipukizi wa mitaani –wenye majumba katika barabara ukingoni mwa bandari,wanafunzi na punks.Sven Brux,ambae leo ana dhamana ya usalama katika uwanja wao wa Millentor aliandaa mila maalumu kwa klabu hii.Anakumbusha Brux:

“Klabu ya St.Pauli wakati ule haikuwa na zaidi ya beji ya klabu yao,mafla na a.lama za utambulisho za kubandika…”

Kipenzi cha mashabiki zama zile alikuwa kipa Volker Ippig na kwa muda mrefu akiishi kandoni mwa njia ya bandari ya st.Pauli.Ippig aliwahi kutumika katika misaada ya maendeleo ya kuijenga upya Nicaragua.”

“ Sikuwa mwenye siasa kali hivyo.Ni khadithi tu zilizokuwa zikisimuliwa juu yangu kinyume na nilivyo.Nilipokwenda Nicaragua au nilipoishi katika njia kandoni na bandari huko St.Pauli nilikua bado sifanyi kazi kama kipa wa kulipwa-prof.”

FC st.Pauli iliundwa Mai 15, 1910. Tarehe muhimu katika historia ya klabu hii lakini ni Dezemba 26,1952,kwani siku hiyo kwa mara ya kwanza mchezo wa kwanza wa dimba ulioneshwa katika TV ya Ujerumani-nao ulikua kati ya FC st.Pauli na Harborn 07.Ni kiasi cha watu 4000 waliokuwa na TV nchini kote Ujerumani enzi zile.Uwanjani kulikuwa na mashabiki 4.500 waliojionea st.Pauli ikilazwa mabao 4:3 baada ya kurefushwa mchezo.

Katika msimu wa 1975/76,FC st.Pauli kwa mara ya kwanza ilipanda daraja ya kwsanza ya Bundesliga kabla hakikuingia kipindi cha kupanda na kushuka.Mara ya mwisho St.pauli kupanda daraja ya kwanza ilikua Mai 2001.

“na sasa wachezaji waliovalia jazi za kahawia na nyeupe, wauvamia uwanja wakikumbatiana,kwani wahamburg wameshinda mabao 2:1 .Na hii ni mara ya 4 katika historia yao kupanda daraja ya kwanza.”

Lakini alie juu mngoje chini,kwani haukupita muda FC st.pauli ilitoka daraja ya kwanza hadi ya 3 na iliepuka kufilisika kabisa hapo 2003.Rais wake Corny Littmann,aliiokoa St.Pauli.Alitengeza fulana-T-shirts 140.000 akiwataka mashabiki kununua kuikoa St.Pauli.

Chini ya rais Littmann,St.Pauli ilijenga heba na jina jipya.Uhasama wa kale na wa muda mrefu na bayern munich pamoja na meneja wake Uli Hoeness ukazikwa .

FC St.Pauli itakumbukwa ilikua klabu ya kwanza kuitikia barua wazi iliochapishwa na wachezaji 3 wa kiafrika-Anthony Bafoe na Anthony Yeboah (Ghana) na Suleiman sane (Senegal) kupinga bughdha za ubaguzi na matusi viwanjani kwa wachezaji weusi.

St.Pauli ilianzisha kampeni ya kupinga ubaguzi wa kila aina.

FC st.Pauli,klabu ya Bundesliga ilioasisiwa 1910 ingali hayi na msimu ujao inarudi daraja ya pili ya Bundesliga kutoka ya 3 na mambo yakienda uzuri, huenda kama 2001 ikapanda tena daraja ya kwanza ya Bundesliga.