1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yampiga marufuku Luis Suarez

Admin.WagnerD27 Juni 2014

Shirikisho la FIFA, limemfungia mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez kucheza michezo tisa ya kimataifa pamoja na kushiriki katika shughuli zozote zinazohusiana na mchezo wa soka kwa kipindi cha miezi minne

https://p.dw.com/p/1CRK0
Fifa WM Italien Uruguay Chiellini Bissspuren Suarez
Picha: picture-alliance/dpa

Hii ni baada ya kumkuta mshambuliaji huyo wa klabu cha Liverpool cha England na hatia ya kumng'ata begani mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini wakati wa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi baina ya miamba hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la soka duniani FIFA, Delia Fischer amesema adhabu ya Luis Suarez inaanza mara moja na mshambuliaji huyo ataukosa mchezo wa hatua ya 16 bora katik ya timu yake ya Uruguay na Colombia aidha anatarajiwa kukosa zaidi ya michezo 30 ya ligi kuu ya Uingereza kutokana na kufungiwa kushiriki katika matukio yoyote ya michezo ikiwemo kuingia viwanjani.

Ghana yawatimua Muntari na Kevin Prince Boateng

Tukiliweka kando hilo ndoto za timu ya taifa ya soka ya Ghana za kutinga katika hatua ya 16 bora katika fainali tatu mfululizo za michuano ya kombe la dunia zipo mashakani baada ya shirikisho la soka la Ghana, GFA kuwaondoa kwenye kikosi Kevin Prince Boateng pamoja na Sulley Muntari kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Taarifa ya GFA imeeleza kuwa, Muntari alimpiga mjumbe wa utendaji wa shirikisho hilo Moses Armah wakati wakikao cha wachezaji na viongozi. nae Kevine Prince Boateng alimtusi kocha mkuu wa Black Stars Kwesi Appiah wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Mwandishi: Anuary Mkama/AFP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman