1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA: Wagombea watano wa urais waidhinishwa

12 Novemba 2015

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limeidhinisha wagombea watano katika uchaguzi utakaofanyika Februari mwakani kuchukua nafasi inayoachwa wazi na rais wa sasa aliyesimamishwa kazi Sepp Blatter

https://p.dw.com/p/1H4Qe
FIFA Symbolbild
Picha: picture-alliance/dpa/E. Leanza

Wagombea hao watano ambao wametimiza masharti kufuatia usaili kuhusu maadili ni pamoja na mwanamfalme Ali Al Hussein wa Jordan, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, Jerome Champagne, Gianni Infantino na Tokyo Sexwale wa Afrika kusini.

Kiongozi wa shirikisho la kandanda barani Ulaya Michel Platini, ambaye amesimamishwa uongozi alikuwa mmoja wa watu waliopewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, atafanyiwa tathmini mara baada ya muda wake wa kusimamishwa kwa siku 90 kumalizika.

Rais wa Shirikisho la Kandanda la Ulaya – UEFA aliyeachishwa kazi kwa muda pamoja na Blatter, Michelle Platini, na Rais wa shirikisho la kandanda la Liberia Musa Bility hawajafaulu kujumuishwa katika orodha ya wagombea watano wa mwisho.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman