1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FLORIDA: Watu kumi na tisa wafariki kutokana na kimbunga, Florida, Marekani.

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVh
Watu kiasi kumi na tisa wamefariki na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya mvua kubwa na kimbunga kupiga maeneo ya jimbo la Florida nchini Marekani.

Karibu nyumba mia tano zimeharibiwa.

Makundi ya waokoaji yanawatafuta walionusurika au walionaswa kwenye vifusi vya nyumba zao.

Wateja kiasi elfu ishirini wamekatiziwa huduma ya nguvu za umeme katika eneo la Florida ya kati.