1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frank-Walter Steinmeier, mgombea wa kiti cha Kansela wa Ujerumani

Nijimbere, Gregoire19 Oktoba 2008

Chama cha Social Democratic kimemteua mwakilishi wake kwenye uchaguzi wa Kansela wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/FcrA
Frank- Walter SteinmeierPicha: AP

Katika mkutano maalum mjini Berlin, chama cha Social Democratic cha SPD nchini Ujerumani kimemteua Frank- Walter Steinmeier kuwa mgombea wake wa kiti cha Kansela wa Ujerumani katika uchaguzi uliyopangwa kufanyika mwakani. Steinmeier amepitishwa kwa asili mia 95 ya kura.

Katika hutuba yake, makamu wa sasa wa Kansela wa Ujerumani aliyepia waziri wa mambo ya kigeni, amewatolea wito wajumbe kwenye mkutano kukiunga mkono chama.

Frank Müntefering aliyewahi kuwa kiongozi wa chama hicho cha SPD, amerejeshwa kwenye uongozi wa chama baada ya kujitenga na mambo ya kisiasa kiasi cha mwaka moja uliyopita. Wafuasi wa chama cha Social Democratic wanatumai wanasiasa hao wawili wataweza kuigeuza hali ya hivi sasa ya chama ambacho kimeshuka katika kura za maoni.