1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT AM MAIN: Klein amerejea Ujerumani baada ya kuwa jela Iran

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ7

Mjerumani Donald Klein amerejea Ujerumani baada ya kuwa jela kwa takriban miezi 16 nchini Iran. Kwa mujibu wa polisi,Klein alie na umri wa miaka 53 aliwasili uwanja wa ndege wa Frankfurt-am-Main ambako alipokewa na familia yake.Klein alikamatwa Novemba mwaka 2005,baada ya kuingia katika bahari ya Iran akiwa katika mashua ya tanga.Baada ya kufikishwa mahakamani,Klein alipewa kifungo cha jela cha mwaka mmoja na nusu hapo Januari 2006.Aliachiliwa huru siku ya Jumatatu mjini Teheran.