1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN : Mpinzani Koroma aongoza uchaguzi wa rais

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZ7

Mgombea mkuu wa upinzani anaongoza katika uchaguzi wa rais nchini Sierra Leone wakati matokeo ya kwanza yakitolewa hapo jana.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliotolewa na Tume ya Uchaguzi hapo jana wakati asilimia 19 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa Ernest Bai Koroma amejipatia kura 204,774 ambazo ni maradufu ya zile alizopata mgombea wa chama tawala makamo wa rais wa nchi hiyo Solomon Berewa aliyejipatia kura 106,487.

Mshindi anahitaji asilimia 55 ya kura ili kuepuka marudio ya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo wa kwanza kufanyika tokea kuondoka nchini humo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa miaka miwili iliopita kwa wengi wanauhesabu kuwa ni fursa kwa nchi hiyo kuthibitisha kwamba ni taifa lenye demokrasia inayofanya kazi baada ya kuondokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.