1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN:Mtumbwi wazama pwani ya Sierra Leone

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcW

Yapata watu 21 hawajulikani waliko baada ya mtumbwi mmoja uliosafirisha abiria kwenye pwani ya eneo la kusini nchini Sierra Leone kuzama.Boti hiyo ilizama kwenye kijiji cha Bailor ilipokuwa safarini kutoka mji mkuu wa Freetown na kuelekea mji wa Kasirie.

Hayo ni kwa mujibu wa naibu kiongozi wa polisi Mustapha Kamara.Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu mkasa huo.