1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN:Wananchi wa Siera Leone waendelea na upigaji kura.

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaB

Wananchi nchini Siera Leone leo wamepiga kura katika uchaguzi mkuu wa raia na wabunge toka vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vilipoondoka nchini humo miaka miwili iliyopita.

Watu wengi walijitokeza toka mapema alfajiri katika vituo vya kupigia kura, huku hali ya usalama ikiimarishwa.

Kuna wagombea saba wanaowania kiti cha urais kinachoachwa wazi na Rais Ahmed Tejan Kabbah anayeng´atuka kwa mujibu wa katiba baada ya kutumikia vipindi viwili vya miaka mitano mitano.