1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN:watu 20 wafa katika ajali ya helikopta

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv2

Habari kutoka Sierra Leone zinaarifu kwamba helikopta moja iliyokuwa inawasafirsha watu hadi uwanja mkuu wa ndege wa Freretown imeanguka na kuwauwa takriban watu 20.

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema kuwa mashabiki wa timu ya mpira ya Togo iliyokuwa imeishinda timu ya Sierra Leone katika mechi ya kuwania klabu bingwa Barani Afrika ndio waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo.

Mmoja wa marubani wa helikopta hiyo amenusurika kifo lakini amejeruhiwa.