1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fury vs Klitschko sehemu ya pili

9 Aprili 2016

Tyson Fury atatetea mataji yake ya dunia ya WBA na WBO katika mchuano wa marudio dhidi ya Wladmir Klitschko mjini Manchester mnamo Julai 9.

https://p.dw.com/p/1ISSP
Boxen Schwergewicht Wladimir Klitschko - Tyson Fury
Picha: picture alliance/Sven Simon/F. Waelischmiller

Hayo yametangazwa na mwalimu wa bondia huyo Muingereza ambaye pia ni mjombake Peter Fury

Klitschko mwenye makaazi yake mjini Hamburg, Ujerumani, alipoteza mataji yake ya WBA, IBF na WBO dhidi ya Fury kupitia wingi wa pointi katika pigano lao la Dusseldorf mwezi Novemba mwaka jana. Kilikua kichapo cha kwanza kwa Muukraine huyo katika zaidi ya muongo mmoja. Fury aliye na umri wa miaka 27, anayetokea Manchester, kaskazini ya England, alipokonywa mkanda wa IBF kwa kukubali kupanda ulingoni na Klitschko katika mpambano wa marudiano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/Reuters/DPA
Mhariri: Sessanga Iddi