1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G-8-kundi la dola nane tajiri duniani

25 Mei 2007

Kundi la G-8 halitimiza ahadi lilzotoa kwa nchi masikini kuongeza maradufu misaada yao. Ndio zimezifutia baadhi ya nchi masikini madeni yao, lakini msaada wa maendeleo wakati huo huo umepungua kwa kima cha 2%.

https://p.dw.com/p/CHDj

Kundi la dola kuu 8 Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo (OECD) linatarajia uchumi wa Ujerumani utazidi kukua.Mabingwa wa kiuchumi nao wanatumai uchumi huo, utakua kwa zaidi ya kima cha 2.9%.

Hata Marekani, haoneshi kutakuwa na upungufu wa fedha,kwani jana Bunge limeidhinisha bajeti ya mabilioni kugharimia vita vya Irak.Hatahivyo, licha ya utajiri wao dola hizo 8, hazikutimiza ahadi zao zilizotoa kwa nchi masikini:

Dola kuu 8 tajiri hazikutimiza ahadi zilizotoa huko Greeneagles-licha ya kuwa kwao wao fedha hizo ni sawa na njugu-nyasa.

Chini ya shabaha ya Millenium,ulimwengu uliekeana ahadi kuupiga vita umasikini na maradhi.Shabaha iliotolewa mwaka 2000, ilikuwa kupunguza maafa hayo kwa nusu hadi ifikapo 2015.Hadi sasa lakini, dola hizo tajiri hazikutimiza ahadi zao.

Mfadhili mpya akijitokeza kama vile china,Marekani na Ulaya, huanza kurudi nyuma katika ahadi zao binafsi kwa masikinitena tangu Afrika hata Asia.

Kwa njia hii heba ya dola kuu 8-tajiri inaanza kuingia dosari ikiwa zinashindwa kutimiza ahadi zilizotoa.

Ingawa kundi la G-8 katika kikao chake huko Gleeneagles,Scotland 2005 zililiahidi bara la Afrika kuliongezea misaada maradufu,hakuna mpango wowote ulioibuka vipi zinapanga kufanya hivyo.

Mwaka wa kwanza baada ya mkutano wa Gleeneagles,hesabu zilifunikwa-funikwa kupitia kufuta madeni ya baadhi ya nchi hizo.

Na sasa baada ya kufutiwa madeni nchi hizo, ukweli umedhihirika dhahiri-shahiri:Msaada wa maendeleo kwa Afrika na kwa nchi masikini kabisa kwa jumla, umeteremka mno.Bila ya kuzifutia madeni nchi hizo, misaada kwa Afrika nzima kati ya 2005 na 2006 uliongezeka kwa kima cha 2%.Kima hiki kiko mbali sana na ahadi ya kuongeza misaada maradufu.

Msaada rasmi wa maendeleo kwa nchi zote zinazopokea msaada bila ya kufutiwa madeni,uliteremka kwa kima cha 2%.Hata Banki kuu ya Dunia ambayo huwatetea wafadhili, imeungama kwamba ahadi za kuzisaidia mno nchi masikini hazikutimizwa.

Ili sasa kuokoa jina na heshima yao,dola kuu 8 tajiri duniani, hazimudu tena kutoa porojo tupu-vitendo vyapasa kuonekana.

La kwanza kabisa, zinapaswa kubainisha wazi kwamba zina nia kweli ya kutekeleza ahadi zao kuwa msaada kwa Afrika hadi ifikapo 2010 utapandishwa kwa kima cha dala bilioni 25 na kufikia dala bilioni 50 kwa mwaka.Pili, kundi la G-8 litabidi kupitisha mpango madhubuti wa kivitendo.

Kutotoa ahadi madhubuti kwa kila nchi katika kundi hilo la dola kuu 8, kunakasirisha na kuabisha serikali.Tatu, nchi zinazopokea misaada zinapaswa kuelewa nazo msada zinazopewa utaongezeka kwa kima gani kila mwaka ili ziweze nazo kutunga mipango yao hadi 2010.