1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"G8 haina maana"-wanasema wapinzani wa utandawazi

Oummilkheir6 Juni 2007

Wapinzani wa utandawazi wanataka mikutano ya kilele ya G8 ikome

https://p.dw.com/p/CB3k
Kambi ya wapinzani wa utandawazi mjini Rostock
Kambi ya wapinzani wa utandawazi mjini RostockPicha: picture-alliance/ dpa

Duru kumi za majadiliano na warsha 120-hiyo ndio ratiba ya mkutano badala unaofanyika tangu jana mjini Rostock wakiuhudhuria wapinzani wa utandawazi.Wanataka kubainisha upinzani wao dhidi ya mkutano wa kilele wa G8 mjini Heiligendamm.Mada mazungumzoni zinaanzia “Kazi ya akinamama na utandawazi,kupitia ushirikiano pamoja na bara la Afrika hadi kufikia juhudi za kujiimarisha kijeshi barani Ulaya. Mmojawapo wa wahubiri mashuhuri wa mkutano huo wa Rostock ni professor wa sosiolojia wa Philippines.-mshindi wa zawadi badala ya amani ya Nobel,Walden Bello.

Kwa maoni ya Walden Bello mkutano wa kilele wa G8 mjini Heiligendamm si chochote chengine isipokua porojo tuu.Mkutano huo wa wababe wa dunia hauna haki yoyote-analalamika profesa huyo wa sosiolojia kutoka Philippines,anaetajikana kua mkosoaaji mkubwa wa utandawazi:

“Hakuna hata ahadi moja iliyotolewa miaka ya nyuma na viongozi wa G8 iliyotekelezwa-naiwe panapohusika na haaki sawa kati ya nchi za kaskazini na zile za kusini au katika masuala ya kuhifadhiwa hali ya hewa au kufutwa madeni ya nchi masikini duniani.Maneno matupu tuu.”

Akivalia suruwali ya jeans na shati la miraba,bwana huyo mfupi na mpole amesimama kidete kupigania msimamo wake.Na msimamo wake ni huu:”Utandawazi haujaziletea nchi za kusini neema iliyokua ikitegemewa ,badala yake utandawazi umezidisha hali ya umaskini na kuzifanya nchi hizo zizidi kutegemea misaada kutokqa nje.Ndio maana Bello anataka utandawazi ubadilishwe:badala ya kuwepo biashara huru isiyojali mipaka,anapendelea watu watafakari na kurejesha utaratibu wa zamani wa kiuchumi.Haimaanishi lakini kwamba harakati za uchumi wa kimataifa zitaachiliwa mbali au vizingiti vya aina mpya kujengwa.Kipa umbele kinatakiwa kituwame katika mahitaji ya kitaifa.Hakuna haja ya kuwepo taasisi kuu yoyote eile kwasababu taasisi kama hiyo haisaidii chochote isipokua kuzidisha nguvu za mataifa tajiri .

Ndio maana Walden Bello anataka taasisi kama kwa mfano fuko la shirika la fedha la kimataifa,IMF,benki kuu ya dunia au shirika la biashara la kimataifa-WTO zitoweke,sawa na anavyopendelea ikome mikutano ya kilele kama huu wa G8.

“Tutabidi tuchunguze kwa makini kitakachotokana na mkutano wa kilele wa Heiligendamm-lakini si hasha kwamba asili mia 95 ni maneno matupu.Angalia,yote yaliyoahidiwa katika mkutano mkuu wa Gleneagles mwaka 2005,hakauna hata kimoja kilichotekelezwa!Ndio maana nnafikiri mie bora tukaachana na G8.Nataraji huu utakua mkutano wa mwisho wa kilele wa G8.

Walden Bello ni mgeni wa heshima katika mkutano huu badala wa mjini Rostock wakihudhuria wawakilishi wa mashirika yanayopinga utandawazi,mashirika yasiyomilikiwa na serikali NGO’s,mashirika yanayotetea haki za wafanyakazi,wanaharakati wanaopigania amani na mashirika mengineyo ya kanisa.Walden Bello anashiriki katika warsha na mijadala kadhaa.Jumla ya maonyesho 130 yatafanyika katika kipindi cha siku tatu.

Walden Bello anaamini chombo kama hiki cha G8,itafika siku tuu kitavunjika.Kwasababu anasema fikra asilia iliyopelekea kuundwa G8 –yaani kuwepo kituo cha kusimamia shughuli za kiuchumi za mataifa yenye nguvu,haijaleta tija.Sababu kubwa ya hali hiyo anasema Walden Bello,inatokana na hali ya kujipendelea na hasa ya Marekani.