1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaidi Klar atabakia gerezani

8 Mei 2007

Baada ya mjadala mrefu wa hadhara, jana usiku rais Horst Köhler wa Ujerumani alitoa uamuzi wa mwisho: Alikataa kumpa msamaha gaidi wa zamani, Christian Klar, wa kundi la kigaidi lilokuwa na msimamo mkali wa mrengo wa kushoto, RAF.

https://p.dw.com/p/CB4E
Rais Horst Köhler, gaidi Christian Klar
Rais Horst Köhler, gaidi Christian KlarPicha: AP
Ombi hilo na kupewa msahama lilizusha mivutano juu ya vipi kuwatendea magaidi kutoka kundi ambalo haliko tena siku hizi nchini humu. Basi, je, uamuzi huo wa rais ulifaa? Ufuatao ni uchambuzi wa mwandishi wetu wa masuala ya ndani, Heinz Dylong:

Hakuna shaka yoyote juu ya Christian Klar: Alikuwa mmoja wa magaidi makali zaidi wa kundi la RAF. Kukamatwa kwake mnamo Novemba mwaka 1982 kulijibiwa na hisia za kupumua kati ya Wajerumani baada ya mauaji mengi yaliyosababishwa na kundi hilo la kigaidi.

Kwa hivyo sasa ni wazi kwamba Bw. Klar hatasamehewa. Bado ana mwaka mmoja na nusu hadi aachiliwe huru kwa dhamana ikiwa mahakama itaamua hivyo. Ombi la kupewa msahama, Klar alishalipeleka kwa rais miaka michache iliyopita, kabla ya Horst Köhler kuteuliwa. Sasa lakini Rais Köhler alikataa kumseheme, baada ya kuchunguza kwa dhati jambo hili. Horst Köhler alizingatia maoni ya waziri wa sheria na mwendeshaji mashtaka wa serikali. Vilevile alisoma ripoti ya tathmini juu ya mfungwa Klar pamoja na kuzungumza na jamaa wa wahanga wa kundi la RAF. Hatimaye rais alikutana na gaidi huyu mwenyewe. Kwa hivyo uamuzi huo haukuwa jambo rahisi wa rais. Kwa sababu hiyo hakupaswa kabisa kulaumiwa na chama cha kihafidhina cha CSU ambacho kilidai Köhler hatachaguliwa tena ikiwa atampa msamaha gaidi Christian Klar.

Basi, Köhler hakumpa msamaha. Licha ya kuwa ana uhuru wa kuamua mwenyewe, bado anaweza kukosolewa kwa uamuzi huo. Ni wazi kwamba – na ripoti inasema hivyo hivyo kwamba Klar ambaye sasa ana umri wa miaka 54 hatawafyetulia risasi tena wanasiasa au wanauchumi. Mahakama itakayoamua baada ya mwaka mmoja na nusu juu ya kuachiliwa huru kwa dhamana au la, itatumia msingi huo huo. Bado Christian Klar ni mpinzani wa mfumo wa ubepari – lakini maoni yake tu si uhalifu. La muhimu ni hisia za jamaa wa wahanga. Maisha ya mtu hayawezi kulipiwa, si kwa kumfunga gerezani mhalifu miaka 24 au miaka 26.

Miaka 30 iliyopita Ujerumani ulipambana na hali ngumu ya kijamii kutokana na ugaidi wa kundi la RAF, kwani magaida hawa, wauaji na watekaji nyara walikuwa watu kutoka katikati ya jamii hiyo. Hadi leo mzozo huo upo ukiangalia mjadala mkali juu ya ombi la msamaha la Christian Klar. Huenda kumsamehe kungesaidia kutuliza hali na kuviponyesha vidonda vya zamani. Si ni hatua ya kushangaza kwamba adui wa serikali ambaye aliupinga vikali utawala wa nchi hii sasa amemuomba mkuu wa serikali hiyo hiyo imsemehe?