1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gates akosoa washirika wake Afghanistan kwa mafunzo duni

17 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cr6t

WASHINGTON:

Waziri wa Ulinzi wa Marekani- Robert Gates- amevikosoa vikosi vya NATO, vilivyoko kusini mwa Afghanistan ,akisema havikujitayarisha vilivyo kupigana vita vya kuvizia.

Askari wengi kutoka Uingereza,Canada na Uholanzi wako kusini mwa Afghanistan na ndio wanakipata pata cha moto, kutoka kwa wapiganaji wa Kitaliban.Ukosoaji wa Gates umewashangaza wengi katika shirika la kujihami la NATO na pia miongoni mwa washirika wa Marekani.Umekuja siku moja baada ya Marekani kuamua kutuma askari zaidi 3,200 nchini Afghanistan.Kwa mda huohuo Ujeruamni inatathmini kutuma kikosi cha watu 240 kaskazini mwa Afghanistan ili kuchukua pahala pa kikosi cha Norway ambacho kinaondoka huko mwezi julai.