1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gavana wa Benki Kuu Tanzania atimuliwa

10 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cnpa

ARUSHA

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amemtimuwa mkuu wa Benki Kuu nchini humo baada ya kutoweka kwa zaidi ya dola milioni 120.

Philemon Luhanjo katibu wa ofisi ya Rais ameiambia televisheni ya taifa kwamba Rais amekasirishwa sana na upotevu huo ambao ulifichuliwa na shirika la ukaguzi wa mahesabu la kimataifa la kujitegemea la Ernst and Young.

Luhanjo amesema wakaguzi hao wa mahesabu wamebainisha kwamba banki hiyo imejaza hati za malipo ya uongo zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 120 kwa kampuni 22 za ndani ya nchi nyingi zao zikiwa hazipo nchini humo au ni kampuni hewa.

Rais Kikwete ameahidi kwamba wale waliohusika na upotevu huo wa fedha watashtakiwa.

Gavana huyo alietimuliwa Daudi Ballali yuko hospitalini nchini Marekani.