1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Afisa ashambuliwa kwa risasi.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgu

Gari ya afisa mwandamizi wa usalama nchini Palestina imeshambuliwa kwa risasi katika mji ulioko katika eneo la Gaza wa Rafa.

Maafisa wa hospitali wamesema kuwa mtu huyo hakujeruhiwa lakini mlinzi wake na msichana mmoja wamepatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi.

Hakuna kundi lililodai kufanya tukio hilo, lakini inaonekana kuwa tukio hilo ni hali iliyoko hivi sasa ya mapambano ya makundi hasimu kati ya wapiganaji wa Hamas na majeshi ya usalama yanayomuunga mkono rais Mahmoud Abbas.

Wakati huo huo , watu wenye silaha wanaomuunga mkono Abbas wamefyatua risasi dhidi ya wanachama wa Hamas katika mji wa ukingo wa magharibi wa Nablus, na kuwajeruhi karibu watu tisa.