1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Chama cha Hamas chatoa wito mwandishi wa habari aachiwe huru.

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrN

Tawi la kijeshi la chama cha Wapalestina cha Hamas limetoa wito mwandishi wa habari raia wa Uingereza, Alan Johnson, aachiwe huru mara moja.

Mwandishi huyo wa habari alitekwa nyara mjini Gaza miezi mitatu iliyopita.

Tawi la Ezzedine al-Qasam limesema litachukua hatua mwafaka kuhakikisha mwandishi huyo wa habari ameachiwa huru.

Alan Johnson, ambaye ni mwandishi wa habari wa BBC, alitekwa nyara na kundi linalosemekana kuwa na uhusiano na chama cha Hamas.