1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY.Mapigano yazuka upya Ukanda wa Gaza

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7ED

Mapigano mapya yamezuka leo hii kati ya vikosi vya polisi vya Hamas katika ukanda wa Gaza na ukoo wenye nguvu unaoegemea upande wa chama cha Fatah.

Duru za hospitali katika eneo hilo zimearifu kwamba watu kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Mapigano kama hayo yalizuka pia siku ya jumatano kati ya ukoo huo wa Hellis na vikosi vya askari wa Hamas ambapo watu wanne waliuwawa na wengine 30 wakajeruhiwa.

Mapigano hayo ndiyo mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu Hamas lilipochukua madaraka katika ukanda wa Gaza.