1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Ghasia zasitisha mashauriano kati ya Hamas na Fatah.

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXZ

Watu kiasi kumi na watatu wameuawa kwenye mapigano kati ya makundi hasimu ya Wapalestina kwenye ukanda wa Gaza na kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Idadi hiyo ya watu waliouawa ndio kubwa zaidi iliyotokana na ghasia za wenyewe kwa wenyewe za Wapalestina kwa siku moja, tangu chama cha Hamas kiliposhinda uchaguzi mkuu mwaka uliopita.

Msemaji wa Hamas, Ismail Radwan, amesema chama chake kimechukua hatua hiyo kuonyesha upinzani wake dhidi ya mapigano hayo.

Ghasia zilianza wakati maelfu ya wafuasi wa Hamas walipoandamana katika ukanda wa Gaza kusherehekea mwaka mmoja tangu chama hicho kiliposhinda uchaguzi dhidi ya chama cha Fatah kinachoongozwa na Rais Mahmoud Abbas.

Kwa sasa hivi, wapatanishi wanashauriana na chama cha Fatah ili kuhakikisha kuachiliwa huru wafuasi kumi na tisa wa Hamas waliotekwa nyara na wanamgambo wa Fatah wakati wa ghasia hizo.

Pande hizo mbili zimekuwa zikishauriana kwa majuma kadhaa kwa nia ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.