1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Hakuna maafikiano kuhusu serikali mpya ya Wapalestina

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMG

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas amekutana na waziri mkuu Ismail Haniyeh mjini Gaza kwa majadiliano ya kuunda serikali ya umoja wa taifa, bila ya mafanikio.Mwezi uliopita,nchini Saudi Arabia,chama cha Fatah cha Abbas na chama tawala Hamas cha Haniyeh,vilitia saini makubaliano ya kugawana madaraka.Makubaliano hayo yamesitisha mapigano kati ya pande hizo mbili lakini yameshindwa kutimiza masharti ya nchi za magharibi ili kuondosha vikwazo vya misaada ya fedha vinavyowaumiza Wapalestina kiuchumi.Maafisa wa Kipalestina wa ngazi ya juu wamesema, majadiliano ya hivi sasa yataendelea kwa siku chache zijazo na kuongezea kuwa pande hizo mbili hazikuafikiana kuhusu nyadhifa kadhaa.Muda wa majuma matano uliopangwa,ili kufanya majadiliano ya kuunda serikali mpya ya umoja wa taifa, unamalizika tarehe 21 mwezi Machi.