1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Hamas na Fatah wakubali kuweka chini silaha

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVW

Makundi hasimu ya Kipalestina Hamas na Fatah, yamekubaliana upya kuweka chini silaha,baada ya kuwa na mapigano makali ya siku mbili katika Ukanda wa Gaza.Si chini ya watu 20 wameuawa katika kipindi cha saa 24 za nyuma.Chini ya upatanishi wa Misri,makundi hayo mawili sasa yamekubali kuwaondosha mitaani wanamgambo wake. Hata hivyo lakini,mashahidi wanasema,hapa na pale,milio ya risasi ilisikika.Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah,mara kwa mara alitoa miito ya kukomesha mapigano. Wakati huo huo Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia, amewahimiza Abbas na kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal kukutana siku ya Jumanne,mjini Mekka na kujariibu kutia saini makubaliano ya kuunda serikali mpya ya Wapalestina yenye umoja wa kitaifa.Mwezi uliopita,Abbas na Meshaal walikutana katika mji mkuu wa Syria,Damascus,lakini walishindwa kuondosha tofauti za maoni zilizokuwepo kati yao.