1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Haniyah arejea nyumbani Gaza.

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjC

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh amefanikiwa kurejea mjini Gaza kutoka Misr baada ya Israel kufunga mpaka kumzuwia kurejea na mamilioni ya dola za msaada. Mlinzi wa Haniyeh ameuwawa katika tukio la kurushiana risasi katika eneo la mpakani la Rafah, na watu kadha wamejeruhiwa , ikiwa ni pamoja na mtoto wa kiume wa haniyeh. Kiongozi huyo wa Palestina amerejea mjini Gaza bila ya fedha hizo za msaada , ambazo Israel inadai zitatumika katika operesheni za kigaidi. Fedha hizo, zilizopatikana kutoka katika ziara ya Haniyah katika eneo la mashariki ya kati, zimebaki nchini Misr na wasaidizi wake. Mamlaka ya palestina imeathirika kutokana na vikwazo vya umoja wa Ulaya na Marekani vilivyowekwa dhidi ya kundi la Hamas kwa kukataa kukanusha matumizi ya nguvu na kuitambua Israel.