1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Haniyeh wa Hamas atoa wito kukutana na Rais Abbas wa Fatah

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp3

Kiongozi wa Hamas,Ismail Haniyeh aliefukuzwa kama Waziri Mkuu wa Wapalestina,ametoa mwito kwa Rais Mahmoud Abbas wa chama hasimu cha Fatah,kufanya majadiliano mapya ya kugawana madaraka.Maafisa wa Fatah,moja kwa moja,waliukataa mwito huo uliotolewa baada ya zaidi ya juma moja,tangu Hamas kudhibiti Ukanda wa Gaza,hatua ambayo Rais Abbas amesema,ni mapinduzi ya serikali.Kwa upande mwingine,Rais Hosni Mubarak wa Misri ameonya, mgogoro kati ya Hamas na Fatah unaweza kuwatenganisha Wapalestina.Vile vile katika ishara kuwa Cairo inawasusa maafisa wa Hamas, Misri imehamisha ubalozi wake kutoka Gaza na umepelekwa Ukingo wa Magharibi.Siku ya Jumatatu, Rais Mubarak atakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele utakaofanywa mji wa kitalii wa Sharm-el-Sheikh kwenye Bahari ya Shamu,nchini Misri. Mkutano huo utahudhuriwa na Rais Abbas wa Wapalestina,Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Mfalme Abdallah wa Jordan.