1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Hatma ya serikali ya Palestina itajulikana leo.

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrm

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, anatarajiwa saa chache zijazo kutangaza hatma ya serikali ya muungano kati ya chama chake cha Fatah na chama cha Hamas.

Msemaji wa Rais Mahmoud Abbas amesema rais huyo anatarajiwa atatoa tangazo muhimu litakaoelezea msimamo wa mwisho wa chama chake kuhusu mzozo huo.

Kumekuwa na tetesi kwamba chama cha Fatah huenda kikajitoa kwenye serikali ya muungano wa kitaifa kutokana na mapigano ya hivi karibuni kati ya wanamgambo wa vyama vyote viwili.

Wanamgambo wa Hamas wanasemekana wamekaribia kulidhibiti eneo lote la ukanda Gaza.

Watu kiasi sitini wameuawa kwenye mapigano ambayo yameendelea kwa siku kadhaa zilizopita.

Mapigano kati ya makundi hayo mawili yamekuwa yakiendelea ingawa Rais Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu Ismail Haniyah wa chama cha Hamas wametoa wito vita vikomeshwe.