1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza: Israel inadaiwa imezuwia kupelekwa mafuta na umeme hadi Ukanda wa Gaza

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bq

Maafisa wa Palastina wanasema Israel imepunguza sana kusafirishwa mafuta hadi Ukanda wa Gaza baada ya kutishia kuweka vikwazo kutokana na mashambulio ya maroketi yanayotokea huko. Lakini Israel, ambayo waziri wake wa ulinzi, Ehud Barak, alitoa amri wiki iliopita kukata usafirishaji wa mafuta na umeme, imesema hatua hiyo bado haijatekelezwa. Wakuu wa Kipalastina wanasema mafuta yaliosafisrihwa leo yamepungua baina ya asilimia 40 na 50 na yale yanayotumiwa na kinu cha umeme cha Gaza kwa asilimia 12. Israel inasema inatumia njia zisizokuwa za nguvu kukimbinya kikundi cha Hamas ambacho kimechukuwa madaraka huko Gaza mwezi Juni ili kusimamisha mashambulio ya maroketi yanayofanywa mpakani na Wapalastina wenye siasa kali.