1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Israil yatangaza italipiza mashambulio ya makombora yanayotokea Gaza

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfr

Israil imeagiza majeshi yake kushambulia vituo vya wanamgambo wa Kipalestina kulipiza mashambulio ya makombora yanayoendelea dhidi yake kutoka ukanda wa Gaza.

Majeshi hayo yatalenga mashambulizi yake kwa wanamgmabo wanaorusha makombora aina ya Qassam kuelekea, nchini Israil kutokea Gaza.

Uumuzi huo umepitishwa baada ya mkutano ulioandaliwa na waziri mkuu, Ehud Olmert, kwa wakuu wa usalama.

Jana usiku wanamgambo wa kipalestina walirusha makombora katika mji wa Sderot, Israil kusini na kuwajeruhi vijana wawili.