1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Israil yawatia nguvuni viongozi wa Wapalestina

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByu

Israil imeendelea na mashambulio ya ndege usiku kucha katika Ukanda wa Gaza na wakati huo huo ikawatia nguvuni wakuu thelathini na watatu wa chama cha Hamas katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Miongoni mwa waliokamatwa ni waziri wa elimu wa Palestina, Nasseredine al-Shaer, wabunge watatu na mameya wanne.

Msemaji wa kijeshi wa Israil amesema watu hao walikuwa wakiunga mkono mashambulio yanayotekelezwa dhidi ya Israil kutokea Gaza.

Wanamgambo wa kipalestina wamekataa wito wa Rais Mahmoud Abbas wasimamishe mashambulio ya makombora dhidi ya Israil, wakisema hawatasitisha mashambulizi yao mpaka Israil kwanza ikomeshe mashambulio yake.

Wakati huo huo mkuu wa sera za kimataifa wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana leo anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israil na Palestina kujaribu kuutafutia suluhisho la kisiasa mzozo huo wa hivi karibuni.