1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Machafuko kati ya Hamas na Fatah yazuka tena

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChH

Mpalestina mmoja ameuwawa katika mapigano mapya yaliyozuka mjini Gaza. Mapigano yameendelea usiku kucha karibu na nyumba ya rais wa Palestina, Mahmoud Abbas na ofisi ya waziri wa mashauri ya kigeni, Mahmoud al Zahar.

Imeripotiwa mapigano hayo kati ya wafuasi wa chama cha Fatah cha rais Abbas na wafuasi wa chama cha Hamas yalianza baada ya watu waliokuwa wamejahami na bunduki kuwateka nyara wanamgambo wawili wa Hamas, akiwemo mlinzi wa waziri al - Zahar.

Wakati haya yakiarifiwa wanamgambo wa kipalestina wamevurumisha roketi katika jangwa la Negev, kusini mwa Israel, licha ya kutangazwa kwa usitishwaji ma mapigano kati ya Israel na Palestina mwezi mmoja uliopita.