1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Majeshi ya Israeli yameanza kuondoka kutoka Gaza wakiviacha nyuma vifo vya watu zaidi ya 50

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv8

Majeshi ya Israeli yameanza rasmi kuondoka kutoka mji wa kaskazini mwa ukanda wa Gaza wa Beit Hanun baada ya operesheni ya wiki nzima ambapo kwa uchache wapalestina 52 na mwanajeshi moja wa Israeli waliuawa. Israeli imesema operesheni hiyo ya kijeshi ililenga kukomesha mashambulizi ya makombora ya wapiganaji wa kipalestina katika maeneo ya karibu nchini Israeli. Lakini vyombo vya habari nchini Israeli vimearifu kuwa kabla ya kuondoka kutoka Gaza, majeshi ya Israeli yamewauwa wapalestina watano wakiwemo wapiganaji wawili.

Wakati huo huo, rais wa Palestina, Mahmud Abbas na waziri wake mkuu, Ismail Haniya, walikuwa na mkutano kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa lakini wameshindwa hadi sasa kuondoa tofauti zao. Miongoni mwa matatizo yaliojiotokeza ni pamoja na ni nani atakaoiongoza serikali hiyo iwapo itaundwa.Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana tena kwa mazungumzo zaidi lakini hawajasema itakuwa lini.