1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Majeshi ya Israil yawaua Wapalestina wawili.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvg

Majeshi ya Israil yamewapiga risasi na kuwaua wavulana wawili wa kipalestina karibu na mpaka kati ya Gaza na Israil.

Wavulana hao wameuawa karibu na makao ya zamani ya mayahudi.

Duru za kipalestina zinasema wavulana hao walikuwa miongoni mwa kundi la watoto waliokuwa kwenye ufukwe wa bahari wakinuia kuogelea.

Majeshi ya Israil yamesema askari wake waliwapiga risasi Wapalestina kadha walioonekana wakitambaa kuelekea kwenye ukuta wa mpaka karibu na mji wa Beit Lahiya.