1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Majeshi ya Palestina yapata silaha.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfV

Majeshi ya usalama yanayomuunga mkono rais wa Palestina Mahmoud Abbas wanaripotiwa kupata silaha ambazo zimesafirishwa kuingia katika ukada wa Gaza kutoka Misr.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa shehena hiyo ya silaha imeidhinishwa na serikali ya Israel.

Ripoti hiyo haikusema wapi silaha hizo zimenunuliwa. Makubaliano tete ya kusitisha mapigano yamefikiwa kati ya chama cha Fatah cha Bwana Abbas na serikali inayoongozwa na chama cha Hamas.

Takriban watu kumi Wapalestina wameuwawa katika ghasia kati ya chama cha Fatah na wapiganaji wa Hamas tangu rais alipotoa wito wa kufanyika uchaguzi na mapema mwezi huu.

Serikali ya Israel, wakati huo huo imeidhinisha matumizi ya mashambulizi ya kulenga ili kuwazuwia wapiganaji wa Kipalestina kurusha maroketi dhidi ya miji ya Israel.