1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Makubaliano mapya ya kusitisha mapigano

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0Z

Makundi hasimu ya Kipalestina,Hamas na Fatah yamekubali kusitisha mapigano ya zaidi juma moja katika Ukanda wa Gaza.Wajumbe wa makundi hayo mawili,katika mkutano uliofanywa kwenye ubalozi wa Misri mjini Gaza,walikubaliana kuwaondosha wanamgambo wao mitaani na kubadilishana mahabusu. Ni mapema mno kusema kama maafikiano hayo yatadumu,kwani makubaliano ya makundi hayo mawili kuweka chini silaha,yalivunjwa mara kwa mara.Hadi watu 50 wameuawa katika mapigano ya juma moja.