1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Makundi ya wapalestina yakubaliana kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpt

Makundi ya wapiganaji wa kipalestina yamekubaliana kusimamisha mapigano na Israel baada ya mazungumzo na waziri mkuu, Ismail Haniya, mjini Gaza. Kiongozi wa kundi la Islamic Jihad kwenye ukanda wa Gaza, Khader Habib, amewaambia waandishi wa habari kwamba wawakilishi kadhaa wa makundi ya kiislamu, wamekutana kwa mazungumzo na waziri mkuu, Ismail Haniya, na kwamba wamekubali kusimamisha mapigano, ikiwa Israel itakubali kufanya hivyo.

Itabidi mapatano hayo yakubaliwe pia na vyama vya Fatah na Hamas.

Ikiwa mkataba huo utakubaliwa na Israel, makundi ya wanaharakati wa kipalestina yatasimamisha mashambulizi yao dhidi ya Israel.

Jeshi la Israel lilianza jumatatu wiki hii operesheni kubwa ya majeshi ya nchi kavu kaskazini mwa ukanda wa Gaza. Operesheni hiyo ambayo bado inaendelea, imeshapelekea mauaji ya watu 12 na majeruhi ya watu zaidi ya 20.