1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Mapigano bado yanaendelea.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzx

Israel imefanya mashambulizi kadha ya anga dhidi ya mji wa Gaza, kwa kujibu mashambulio kadha ya maroketi yanayofanywa na wapiganaji wa Kipalestina.

Hapo mapema majeshi ya ulinzi ya Israel yalirusha kombora katika nyumba moja mjini Gaza, na kuuwa kiasi watu wanane na kuwajeruhi wengine 13.

Duru za hospitali na wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa nyumba hiyo ilikuwa ya mbunge wa chama cha Hamas Khalil al-Haya, ambaye hakuwepo wakati wa shambulio , na kwamba wale waliouwawa ni pamoja na nduguzake sita.

Jengo linalosadikiwa kuwa ni kiwanda cha kutengenezea makombora limeshambuliwa katika shambulio la pili. Waziri wa masuala ya jamii wa Israel Jizhak Herzog amesema kuwa Israel inalazimika hivi sasa kuwalinda raia zake kutokana na mashambulio ya makombora kutoka kwa Wapalestina.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameapa kuzidisha mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya wapiganaji wa Kipalestina.

Wakati huo huo makubaliano ya hivi karibuni kabisa ya kusitisha mapigano baina ya makundi ya Hamas na Fatah yanaonekana kudumu. Kiasi watu 50 wameuwawa katika mapigano hayo ya kimakundi katika muda wa wiki moja iliyopita.