1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mapigano yachacha katika Ukanda wa Gaza.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCX4

Mapigano yameendelea kati ya makundi hasimu, chama cha Hamas na chama cha Fatah, katika Ukanda wa Gaza.

Ghasia hizo tayari zimesababisha vifo vya watu ishirini na wawili tangu Alhamisi usiku.

Wanamgambo wa chama tawala cha Hamas wamevurumisha makombora kwenye makao ya kikosi cha polisi kinachosimamiwa na chama cha Fatah cha Rais Mahmoud Abbas.

Makundi hayo hasimu yamekuwa yakijaribu kwa miezi kadha kuunda serikali ya umoja wa kitaifa lakini mashauriano hayo yamekuwa yakisimamishwa mara kwa mara.

Chama cha Hamas ndicho kilichotangaza kususia duru ya hivi karibuni ya mashauriano siku ya Ijumaa usiku.

Ghasia hizo ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu chama cha Hamas kiliposhinda uchaguzi wa mwaka uliopita.

Serikali ya chama hicho inakabiliwa na vikwazo vya Marekani kwa sababu ya msimamo wake wa kutoitambua Israil.