1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mapigano yaendelea kati ya Hamas na Fatah katika Ukanda wa Gaza.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV6

Mapambano yangali yakiendelea kati ya makundi hasimu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Mapambano hayo yamekuwa yakiendelea ingawa vyama hivyo, Fatah na Hamas, vilikubaliana siku ya Ijumaa kukomesha uhasama.

Afisa wa usalama wa Fatah alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao makuu ya chama hicho.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah, na kiongozi wa Hamas, Khaled Meshall wamekubali kukutana mjini Makkah, Saudi Arabia siku ya Jumanne kujaribu kusuluhisha mzozo huo.