1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza: Mapigano yaendelea kati ya Hamas na Fatah

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiP

licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano , vikundi hasimu vya Hamas na Fattah huko, Palestina, kumeendelea kuwepo kwa mapigano.

Mapema leo asubuhi, mapigano yaliendelea katika wanamgambo wa vikundi hivyo kuwania udhibiti wa serikali ya wapalestina.Mapigano hayo yamefanyika katika makazi ya rais wa mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas.

Hapo jana, msafara wa waziri wa mambo ya nje wa Palestina, ulishambuliwa, ambapo ofisi ya bwana Mahomud Abbas Ilishambuliwa kwa maroketi, katika mapigano ya mchana mkutwa yaliyopelekea watu watatu kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Waziri Mkuu Ismail Haniya amemlaumu hasimu wake Mohamed Abbas wa kikundi cha Fattah kwa kuchochea vurugu, katika mgogoro huo wa kisiasa, kufuatia wito wake kuitisha uchaguzi mapema. Hamas imesema kuwa itaususia uchaguzi huo.

Lakini mwanahataraki mmoja huko Palestina, Moustafa Barghuit anasema kuwa kuitisha uchaguzi si suluhisho la mzozo huo.

Wakati huo, waziri mkuu wa Uingereza, Tonny Blair amewasili nchini Israel, baada ya ziara yake ya siri nchini Iraq.