1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mapigano yazuka tena

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiC

Mapigano yamezuka mapema leo huko Gaza kati ya maofisa wa polisi waliowatiifu kwa chama cha Hamas na wapiganaji wa chama cha Fatah katika hospitali kuu mjini Gaza. Ufyatulianaji wa risasi baina ya makundi hayo umetokea katika lango kuu na ndani ya hospitali ya Shifa mjini Gaza.

Machafuko hayo yametokea siku moja tu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya makundi hasimu ya Hamas na Fatah kutangazwa. Duru za hospitali hiyo zinasema mtu mmoja ameuwawa na wengine wakajeruhiwa katika machafuko hayo.

Mapigano kati ya wafuasi wa Hamas na Fatah yameendelea kuongezeka tangu rais wa Palestina Mahmoud Abbas alipotangaza uchaguzi wa mapema mwishoni mwa juma lililopita.