1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Rais Abbas amevunja serikali ya umoja wa kitaifa

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBra

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah,ameivunja serikali ya umoja wa kitaifa na ametangaza hali ya hatari.Vile vile amemfukuza Waziri mkuu Ismail Haniyeh wa Hamas na amesema ataunda baraza la mawaziri la dharura kuongoza kwa amri.Muda mfupi baada ya kufukuzwa kama waziri mkuu,Haniyeh alitangaza kuwa Rais Abbas amepitisha uamuzi wake kwa haraka.Akasema, atapuuza amri ya Abbas na kwamba serikali yake itaendelea kufanya kazi.Vile vile ametoa mwito kwa wanamgambo wa Hamas kukomesha mauaji ya kulipiza kisasi katika Ukanda wa Gaza uliotekwa na wanamgambo hao.Wakati huo huo alihakikisha kuwa wanamgambo wa Hamas hawataki kuligawa eneo la Ukanda wa Gaza na kuongezea kuwa umma una haki ya kuwa na taifa moja la Kipalestina.Baada ya mapigano makali ya siku sita na zaidi ya watu 110 kuuawa,chama cha Hamas sasa kimedhibiti eneo zima la Ukanda wa Gaza.