1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza: Vikosi vya Hamas vyakabiliana na wanamgambo hasimu.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcz

Vikosi vya usalama vya Hamas vimekabiliana na wanamgambo wa kundi hasimu katika ukanda wa Gaza.

Afisa wa usalama wa Hamas ameuawa na wengine kadha wa makundi yote mawili wamejeruhiwa.

Mapambano hayo yalizuka pale chama cha Hamas kilipojaribu kuwapokonya silaha watu wasioruhusiwa kuwa nazo.

Wakazi wamesema mzozo huo ulianza wakati wafuasi wa Islamic Jihad walipofyatua risasi hewani kusherehekea harusi.

Wakati huo huo, majeshi ya Israil yameuvamia ukanda wa Gaza na yamewaua wapalestina wawili na yakawajeruhi wengi kadhaa.